Sunday, October 31, 2010

UCHAGUZI MKUU TANZANIA

Leo ni siku ya kutengeneza tena Historia yetu ya Safari ya Miaka Mitano ya Serikali fulani. Ndugu zangu watanzania, leo ni siku muhimu ambayo itatufanya tufurahi ndani ya safari hiyo ya Miaka Mitano au tuwe watu wa Huzuni toka JUA KUCHOMOZA HADI KUZAMA.
Tucheze karata yetu si kwa USHABIKI bali kwa kumtanguliza Mungu katika hili ili aweze kutupatia KIONGOZI SHUPAVU. Tusipomtanguliza MUNGU cha moto tutakiona wenyewe. Tutaishia kusema tungalijua! Mshirikishe Mungu naye atakusaidia.
Msimchague mtu kwa sababu alikununulia shati au kitenge. Mpatie kura yako mwenye Uchungu wa kukuletea MAENDELEO YA KWELI.
Mimi simjui ni nani atatuletea MAENDELEO YA KWELI, ila Mungu peke yake anamjua. Kwahiyo tumuombe yeye afanyekazi yake.
NAKUTAKIA AMANI YA KUDUMU NA SIO YA MDOMONI TU.
AMANI YA KRISTO ITAWALE.

No comments:

Post a Comment